Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jaribio la tahadhari ya Tsunami kufanyika leo Ukanda wa Karibia

Jaribio la tahadhari ya Tsunami kufanyika leo Ukanda wa Karibia

Siku ya leo, zaidi ya nchi 31 zinashirikiana katika zoezi maalum la tahadhari ya tsunami, ukanda wa Karibia. Jaribio hilo limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, kupitia Kamisheni ya Kiserikali ya Elimu ya Bahari. Taarifa kamili na  Priscilla Lecomte

(TAARIFA YA PRISCILLA)

Jaribio hilo lilitakiwa kufanyika leo saa nne za asubuhi, saa za Uingereza. Mpangilio wa zoezi hilo ni kuiga tetemeko la ardhi na tsunami, yaliyotokea mwaka 1755, kilomita 430 magharibi mwa Gibraltar. Wakati huo, mawimbi makubwa ya tsunami yalifika Antigua masaa tisa baada ya ardhi kutetemeka.

Vituo vya Tahadhari ya Tsunami vya Mkoa wa Pacifiki na ya Marekani watatuma ujumbe wa bandia kwa nchi zote shirikishi. Lengo ni kutathmini mfumo wa tahadhari ya Ukanda wa Karibia, ambao umeunganishwa mwaka 2005 na nchi za ukanda huu kwa kushirikiana na UNESCO. Waandaaji wa zoezi la leo watahakikisha pia kwamba ujumbe wa tahadhari unapelekwa ipasavyo kwa watu wawajibikaji katika kila nchi, UNESCO ikisisitiza umuhimu wa kasi ya usambazaji wa taarifa kwa kupunguza madhara ya matukiokamatsunami.

Jumla ya matetemeko ya ardhi 75 yametokea katika eneo la Karibia kwa kipindi cha miaka 500, ikichangia asilimia 10% ya matetemeko yote duniani. Eneohilolinakabiliwa zaidi na hatari za matukio ya tabia nchi kutokana na ongezeko la idadi ya watu, na ukuaji wa utalii.