Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR nchini Kenya yashtushwa na tamko la serikali

UNHCR nchini Kenya yashtushwa na tamko la serikali

Shirika la umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR nchini Kenya limesema limeshtushwa na taarifa ya serikali ya nchi hiyo ya kuwataka wakimbizi wote walioko nchini humo kurejea kambini.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii msemaji wa shirika hilo Abel Mbilinyi amesema kufuatia hatua hiyo UNHCR inatarajia kufanya mazungumzo na serikali ya Kenya kwani hatua hiyo imekiuka misingi ya haki na amri ya mahakama iliyotaka wakimbizi waishi popote pale.

( SAUTI MBILINYI )

Akizungumzia namna wakimbizi walivyopokea katazo hilo Bwana Mbilinyi anasema

(SAUTI MBILIBYI )

Tangazo la serikali ya Kenya ambalo lilisisitiza ni kwasababu za kiusalama limefuatia tukio la hivi karibuni mjini

Mombasa ambapo watu sita walifariki dunia baada ya kulipuliwa risasi wakiwa kanisani