Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ziarani Greenland kutathmini athari za mabadiliko ya tabianchi

Ban Ziarani Greenland kutathmini athari za mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, yuko ziarani nchini Greenland kufanya tathmini ya athari za mabadiliko ya tabianchi, kabla ya mkutano wa mkuu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mnamo mwezi Septemba. Joshua Mmali na taarifa kamili

(TAARIFA YA JOSHUA)

Katika ziara hiyo, Bwana Ban anautembelea wa Ilulissat, ulioko kilomita 250 kutoka kwa mzunguko wa eneo la Arctic. Atakutana pia na watu wa jamii ya kiasili ya Uummanaq, ili kuwasikiliza wakizungumzia athari za mabadiliko ya tabianchi katika maisha yao.

Ziara ya Katibu Mkuu inafanyika miezi michache kabla ya mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, wenye lengo la kuchagiza uchukuaji wa hatua za kupunguza vianzo vya ongezeko la joto duniani.

Ban anatarajiwa kuzungumzia kuhusu suluhu buniifu kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi, kama sehemu ya kujiandaa kwa mkutano wa Septemba.