Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aisisitiza kumalizwa kwa mgogoro wa Ukraine kwa njia za kidiplomasia

Ban aisisitiza kumalizwa kwa mgogoro wa Ukraine kwa njia za kidiplomasia

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amesisitiza kuwa mgogoro kati ya Ukraine na Urusi kuhusu jimbo la Crimea utamalizwa kwa njia za kidiplomasia pekee.

Ban ameyasema hayo leo alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron mjini The Hague Uholanzi ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuhusu umuhimu wa kupunguza mvutano nchini humo

Kadhalika katika mazungumzo yao Ban na Camerron wamejadili kuhusu utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia na mkakati maendeleo endelevu baada ya 2015.

Wamesisitiza umuhimu wa kuainisha malengo yakinifu, yanayopimika na yenye mitizamo sahihi kwa ajili ya mkakati wa maendeleo endelevu baada ya 2015.

Katibu Mkuu Ban ameondoka The Hague na tayari amewasili nchini Greenland.