Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watiwa hofu na idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa Misri

UM watiwa hofu na idadi ya watu waliohukumiwa kunyongwa Misri

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza hofu yake juu ya idadi kubwa ya watu waliohukumiwa adhabu ya kunyogwa hadi kufa nchini Misri. Hukumu hiyo ya Jumatatu ni dhidi ya watu 528 na ilitolewa baada ya kesi yao kusikilizwa kwa siku mbili.

Ofisi ya haki za binadamu inasema kesi hiyo haikukidhi viwango vya kimataifa vya kisheria kwani mashtaka dhidi ya watuhumiwa hayakusomwa mahakamani. Halikadhalika upande wa utetezi umeeleza kwamba haukupatiwa muda wa kutosha kuwasiliana na watuhumiwa huku ikiripotiwa kuwa baadhi ya washtakiwa walihukumiwa bila kuwepo mahakamani. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Rupert)