Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wakutana The Hague kujadili hatua za kuzuia ugaidi wa nyuklia

Viongozi wakutana The Hague kujadili hatua za kuzuia ugaidi wa nyuklia

Viongozi wa kimataifa wanakutana mjini The Hague, Uholanzi, kujadili hatua zilizopigwa katika kuzuia ugaidi wa kutumia miyale ya nyuklia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban- Ki-Moon anatarajiwa kuhutubia kikao cha ufunguzi kwenye mkutano huo wa siku mbili unaowaleta pamoja zaidi ya viongozi 50 wa kimataifa.

Mkutano huo unalenga kuhakikisha ushirikiano mahsusi wa kimataifa ili kuzuia magaidi kupata silaha za nyuklia au vifaa vya nyuklia. Mkutano wa kwanza wa usalama wa nyuklia ulifanyika mjini Washington, Marekani mnamo mwaka 2010, kufuatia hotuba ya Rais Barrack Obama iloonya kuhusu hatari ya ugaidi wa nyuklia.