Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WMO yatoa ripoti kuelezea mabadiliko ya tabia nchi

WMO yatoa ripoti kuelezea mabadiliko ya tabia nchi

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la hali ya hewa duniani imeutaja mwaka uliopita wa 2013 kuwa ni wa majanga mazito kwa dunia ukishuhudia matukio kama ukame, mabadiliko ya hali ya hewa na kujitokeza kwa vimbunga vilivyosababisha uharibifu mkubwa wa mali.

Ripoti hiyo pia matukio yaliyojitokeza mwaka huo uliopita yanafanana kabisa na matukio mengine yaliyojitokeza mwaka 2007 ambao ulishuhudia kiwango cha hali joto kikiongezeka zaidi ya mara sita na hivyo kuweka rekodi ya aina yake.

.

(TAARIFA YA GEORGE)

Ripoti hiyo imesema kuwa katika historia ya dunia, karne ya 21 ndiyo iliyoshuhudia matukio mengi zaidi ikiwa kila baada ya kipindi cha muongo mmoja hali ya ujoto ilipanda juu katika kiwango kisichotarajiwa.

Kipindi cha mwaka 2001-2010 ndicho kilichotajwa kuwa kibaya zaidi kutokana na hali ya ujoto kuwa juu zaidi.

Kulingana na mtaalamu wa shirika la hali ya hewa la kimataiifa Michel Jarraud matukio kama mlipuko wa volcano, El Nino na La Nina ni baadhi ya mambo yaliyosababisha kwa hali hiyo.

Bwana Jarraud ambaye ni Katibu Mkuu wa WMO maeneo mengi yalikubwa na hali ya ukame na kwingine kusababisha majanga ya kimazingira kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

(CLIP YA JARRAUD) (HII TUTATOA HUKU