Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW58 yafunga pazia: Shina Inc. yapigia chepuo ubia na elimu kwa jamii kuhusu tamaduni

CSW58 yafunga pazia: Shina Inc. yapigia chepuo ubia na elimu kwa jamii kuhusu tamaduni

Baada ya takribani wiki mbili za vikao kuhusu hali ya wanawake duniani na mustakhbali wa kundi hilo baada ya ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia hapo mwakani na ajenda ya maendeleo endelevu inayofuatia, washiriki wamekuwa na maoni kuhusu mkutano huo uliokutanisha wanawake, wanaume na vijana kutoka kona mbali mbali za dunia. Miongoi mwao ni Jessica Kamala-Mushala kutoka shirika lisilo lakiserikali la Shina linalolenga kukomboa makundi yaliyo hatarini ikiwemo wanawake, vijana na watoto. Akizungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Jessica ametaja umuhimu wa Mwanamke kujitambua na kushirikiana wao wenyewe kwanza ili waweze kusonga mbele. Hapa anaanza kwa kuzungumzia mkutano huo wa CSW.