Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ongezeko la usafirishaji wa madawa ya kulevya Afrika Magharibi laangaziwa.

Ongezeko la usafirishaji wa madawa ya kulevya Afrika Magharibi laangaziwa.

Wakati mkutano kuhusu madawa ya kuleya na athari zake ukiendelea mjini Vienna Austria, usafirishaji wa madawa hayo aina ya cocaine unasalia changamoto kubwa na kumekuwa na ongezeko la kiwango cha usafirishaji wa madawa meingine aina ya heroin katika ukanda huo tangu mwaka 2010.

Hayo ni sehemu ya yaliyojitokeza katika tukio lililoongozwa na kamisheni ya kupinga madawa ya kuleya Afrika Magharibi (WACD) pamoja na muungano wa sera kuhusu madawa haramu (IPDC).

Katika mkutano huo ilibainika kuwa uzalishaji wa madawa aina ya methamphetamine unakuwa Afrika magharibi huku pia usafirishaji wa madawa mengine aina ya ephedrine ukiwa ni jambo la kushughulikwa.

Kwa upande wake rais wa Nigeria Olusegun Obasanjo ameonya kuwa maendeleo yanaleta tishio kubwa la usalama Afrika Magharibi akitolea mfano wa uhalifu wa kupangwa ambapo watekelezaji wake wanatumia ukanda huo kama lango kusafirisha madawa haramu kwenda katika sehemu nyingine za dunia.