Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu Bilioni 1.6 hutegemea misitu kuishi, lazima tuitunze: UM

Watu Bilioni 1.6 hutegemea misitu kuishi, lazima tuitunze: UM

Leo ni siku ya kimataifa ya misitu na miti, ambapo siku hii imetengwa kwa ajili ya kushawishi serikali na wadau kulinda misitu huku wakiimarisha maisha ya wanaotegemea maliasili hiyo ambayo ni theluthi moja ya ardhi duniani kote. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Katika ujumbe wake kwa siku hii Raisi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa John W. Ashe amezingatia faida za misitu kwa mambo ya kiuchumi, kijamii, afya na mazingira., kwa kusisitiza kwamba zaidi ya watu Bilioni 1.6 wanategemea misitu kwa maisha yao ya kila siku.

Ameonya kwamba uharibifu wa misitu umefikia kiwango cha hatari, ambapo zaidi ya hekta milioni 13 za misitu hupotea kila mwaka, na uharibifu huo husababisha kwa asilimia 12 hadi 20 katika utoaji wa gesi chafuzi.

Kwa upande wake Shirika la chakula na kilimo duniani FAO limesema kuna umuhimu wa kufahamu hali ya misitu duniani na kuelewa ni nini kipewe kipaumbele na changamoto. Erik Lindquist ni afisa wa misitu FAO

(Sauti ya Erik)

"Jinsi hali ya ardhi inabadilika ni muhimu kuzungumza na watu wanaotegemea misitu kwa maisha yao ya kila siku na ni muhimu pia katika ngazi ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, upatikanaji wa maji, hewa safi na mvua za kutosha. Haya ni mambo ambayo kwa kawaida hatuazingatii lakini ni muhimu sana."