Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugunduzi wa mafuta Uganda na hatma ya msitu wa Bujaawe yaangaziwa

Ugunduzi wa mafuta Uganda na hatma ya msitu wa Bujaawe yaangaziwa

Tarehe 21 Machi ni siku ya Misitu duniani ambapo Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu Ban Ki-Moon unarejelea wito wa kutaka kutunzwa kwa rasilimali hiyo adhimu kwa maslahi ya dunia zima. Bwana Ban anasema ni vyema kila mtu kutambua na kuzingatia umuhimu wa misitu na kuitumia kiuendelevu kwani athari za matumizi mabaya ya maliasili hiyo sasa ni dhahiri. Je nchini Uganda ugunduzi wa mafuta huko Ziwa Albert unaangaziwa vipi na athari zake kwa msitu wa Bujaawe? Ungana na John Kibego wa Radio washirika Spice FM nchini humo katika makala hii.