Ban akutana na Rais Putin akiwa ziarani Urusi

20 Machi 2014

Katibu Mkuu Ban Kin Moon amewasili nchini Urusi na tayari ameshakutna na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergey Lavrov. Hivi sasa Bwana Ban anakutana na rais wa nchi hiyo, Vladmir Putin kujadili namna ya kuutataua mzozo wa Ukraine.

Awali katika mkutano huo, rais wa Urusi amemshukuru Katibu Mkuu Ban kwa kuongoza juhudi za kutataua migogoro duniani, huku Ban akisema analichukulia kwa uzito suala la mgogoro wa Ukraine na namna Urusi inavyohusika. Ban anatarajiwa pia kukutana na waaandishi wa habari.