Leo ni siku ya kimataifa ya furaha, UM wataka migogoro kukomeshwa

20 Machi 2014

Leo ni siku ya kimataifa ya furaha ambapo bazara kuu la Umoja wa Mataifa lina shughuli maalum kuienzi siku hii hapa mjini New York. Kwa upande wake Katibu Mkuu Ban Kin Moon ametoa ujumbe kuhusu siku hiyo akisema japo furaha yaweza kuwa na maana tofauti lakini wote twaweza kukubaliana kwamba ina maana ya kukomesha migogoro, umasikini na hali zote zisizotarajiwa ambazo binadamu wengi hukumbana nazo.

Bwana Ban amesema hayo yako dhahiri katika mkataba wa Umoja wa Mataifa na kwamba huu niwakati wa kuyatekeleza.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii mjini New York, Kaimu mwenyekiti wa taasisi ya wanawake wabunge nchini Kenya Zeinab Chidzuga anaeleza furaha ina maana gani kwake.

(SAUTI ZEINAB)