Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake lazima washiriki uchaguzi Afghanistan : UM

Wanawake lazima washiriki uchaguzi Afghanistan : UM

Lazima wanawake washirikishwe katika Uchaguzi wa rais na wa halmashauri za kata Afghanistan ili kuhakikisha uchaguzi huo ni wazi na huru, amesema Nicholas Haysom, akiwa ni Naibu Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo na Makamu wa Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa UNAMA.   

Bwana Hayson amesema amefurahi kuona kwamba asilimia 35 ya waliojiandikisha kupiga kura ni wanawake, na kwamba zaidi wa wanawake 300 wamegombea nafasi za halmashauri.

Alitamka hilo baada ya kukutana na wakilishi wa mashirika ya kijamii yanayohusika uwezeshaji wa wanawake.

Amezingatia changamoto ambazo wawakilishi hawa wanakumbwa nazo katika shughuli zao za kila siku, na umuhimu wa jamii katika uwezeshaji wa wanawake wakati wa uchaguzi.

Amesisitiza kwamba ushiriki wa wanawake, wakiwa wagombea, wachunguzi wa uchaguzi au wapiga kura, ni haki ya msingi kwa kila mwanamke, na ni hatua ya lazima kuendeleza demokrasia huko Afghanistan.

Uchaguzi wa rais na wa halmashauri za kata unatarajiwa kufanyika tarehe 5, mwezi Aprili