Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wanawake Afrika bado hawajasaidiwa-Ripoti

Wakulima wanawake Afrika bado hawajasaidiwa-Ripoti

Ripoti mpya iliyotolewa na Benki ya Dunia imesema bara la Afrika liweke usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo iwapo ina nia ya dhati ya kuondokana na umaskini. 

Ripoti hiyo inatokana na utafiti katika nchi za Afrika zikiwemo Ethiopia, Malawi, Niger, Nigeria, Tanzaniana Uganda ambapo uliangalia tofauti ya uzalishaji baina ya wakulima wanawake na wanaume na kusisitiza haja ya kuwajengea uwezo wakulima hao wanawake ambao wanatajwa kuwa na mchango mkubwa katika uzalishaji.

 Katika mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake hapaNew York, suala la wanawake na kilimo linaangaziwa na Cecily Mbarire ni Mwenyekiti wa taasisi ya wanawake wabunge nchini Kenya anazungumziaje hali hiyo?

 (Sauti ya  Cecily)