Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makundi madogo katika jamii bado yapuuzwa: Mtaalamu wa UN

Makundi madogo katika jamii bado yapuuzwa: Mtaalamu wa UN

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za makundi madogo kwenye jamii, ametaka kuchukuliwa kwa hatua zaidi ili kukabiliana na changamoto zinazokabili makundi hayo ambayo amesema yako hatarini kukumbana na vitendo kama vile vya ubaguzi, kukosa fursa za kiuchumi na kukabiliwa na umaskini. George Njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Mtaalamu huyo Rita Izsák amesema kuwa makundi hayo ya watu walioko pembezoni ambayo pia huundwa na watu maskini wa kutupwa yanapaswa kusaidia kujinasua katika hali waliyonayo.

Amesema kutokana na mazingira wanayokumbana nayo, hawawezi kujisaidia badala yake wanapaswa kusaidia kusogezwa mbele.

Mtaalamu huyo ambaye alikuwa akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu alisema kuwa kukosekana kwa mipango mahusisi kwa ajili ya kuwakwamua watu hao kunatia doa juhudi za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

(Sauti ya Rita)

Pia alitolea mfano machafuko yanayoendelea huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusin, Syria na kwengineko akisema kuwa waathirika wa mapigano hayo na watu wa hali ya chini.