Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dokta Kazibwe amweleza Rais Museveni madhara ya sheria dhidi ya Ushoga

Dokta Kazibwe amweleza Rais Museveni madhara ya sheria dhidi ya Ushoga

Wiki tatu baada ya sheria dhidi ya Ushoga kutiwa saini nchini Uganda, Mjumbe maalum wa Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi barani Afrika Dokta Specioza Wandira-Kazibwe amesema amezungumza na Rais Yoweri Museveni na kumweleza madhara ya kitendo hicho kwenye vita dhidi ya Ukimwi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaeleza waandishi wa habari mjini New York kuwa Dokta Wandira-Kazibwe ambaye amewahi kuwa Makamu wa Rais nchini Uganda, amemdokeza rais Museveni kuwa kuharamisha ushoga kunaibua unyanyapaa zaidi na kwamba…

(Sauti ya Dujarric)

Uharamishaji ushoga unachochea unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya wasagaji, waliobadili jinsia na inahatarisha harakati za kitaifa dhidi ya Ukimwi, harakati ambazo zimekuwa zinaleta mafanikio ya dhati.”

Kwa sasa yeyote atakaye patikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja kwa zaidi ya mara moja, atakabidhiwa kifungo cha maisha jela.

Adhabu hiyo pya inawapata wale wanaohushisha watoto, watu wenye ulemavu na wale waliowambukiza virusi vya ukimwi. Kwa Yule atakayepatikana na hatia hiyo kwa mara ya kwanza atakabidhiwa kifungo cha miaka 14