Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali isiposhirikisha walengwa, MDGs zitakamwa: Mshiriki CSW58

Serikali isiposhirikisha walengwa, MDGs zitakamwa: Mshiriki CSW58

Kutoshirikishwa kikamilifu kwa wanachi katika mipango na sera za kitaifa kumesababisha kuchelewa kutekelezwa kwa lengo namba tatu la maendeleo ya milenia kuhusu uwezeshaji wanawake na usawa wa kijinsia

Mkuu wa sera na uwakili wa makubaliano yaliyoko chini ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, UN-Women Selina Sanou kutoka Kenya amesema wananchi wa mashinani wamekuwa hawashirikishwi vya kutosha katika sera za taifa jambo linalokwamisha nafasi ya wanawake na wasichana wakati huu dunia inapoandaa malengo endelevu ya maendeleo baada ya 2015

(SAUTI SELINA)

Hata hivyo Bi. Sanou ambaye ameshiriki mchakato wa kukusanya maoni ya makundi hayo mashinani juu ya nini wanakitaka kihusishwe katika malengo hayo, anataja waliyobaini.

(SAUTI SELINA)