Bila kuwashirikisha wasichana hakuna maendeleo:Washiriki CSW

17 Machi 2014

Katika mahojiano maalum na idhaa hii miongoni mwa waliowasilisha mada waziri wa jinsia kutoka Malawi Mary Mkungwa, amesema ana matumaini mkutano huu utaleta matunda katika ushirikishwaji wa kundi hili na kuongeza kuwa wasichana wapewe kipaumbele kuelekea maelngo endelevu ya milenia baada ya 2015.

(SAUTI MKUNGWA)

Kwangu kitu muhimu ni kwamba tunaongea lugha moja, maendeleo bila wanawake hususani watoto wa kike hayawezekani, kwahiyo jinsi wasichana na wavulana wanavyojihusisha Afrika inakubali tunahitaji kuwa na mbinu sawa kwamba wasichana wanahitaji kushiriki katika kiwango sawia na wanaume. Tunahitaji kumaanisha katika haya tunayosema kwa kuwa mwisho wa siku tunazungumzia malengo endelvu baada ya 2015 na kila nchi inatakiwa kuripoti uhalisia kutoka maendeleo yao, tunahitaji kutengeneza mkakati wa kisheria ambapo wasichana na wavulana watahusishwa.

 

Kwa upande wake msichana Siasi Nyani kutoka Gambia akizungumzia matumaini yake ya ushirikishwaji wa wasichana katika maendeleo endeevu baada ya mwaka 2015 anasema

(SAUTI SIASI)

Kwa sasa nahudhuruia masomo ya utatibu mwaka wa nne, na siku za hivi karibuni tumeona ongezeko la wasichana katika fani hii na fani nyinginevyuoni hata katika elimu za juu tunasona wasichana wengi wanajiunga na masomo ya sayansi pamoja na wavulana. Kwahiyo nafikiri kwa moyo huu na kwa rasilimali tutafika

 

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter