Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujasiriamali waelezwa kuwa muarubaini wa kuwakomboa wanawake kiuchumi

Ujasiriamali waelezwa kuwa muarubaini wa kuwakomboa wanawake kiuchumi

Kujijengea uwezo wa kujitegemea kiuchumi hususani kujikita katika ujasiriamali ni mbinu mbadala ya kuwakomboa wanawake walioko katika katika maeneo ya pembezoni.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii, mwakilishi wa kundi la watu asilia, wamasai kutoka nchini Tanzania Grace Mayasek amesema kufuatia mijadala mbalimbali ya kikao cha 58 kuhusu hali ya wanawake kinachoendela mjini New York, Marekani atahakikisha wanawake katika jamaii anayotoka wanapata elimu kuhusu mbinu za kujikomboa kiuchumi.

(SAUTI GRACE)

Hata hivyo Bi Mayasek amesema msisitizo wa pili utakuiw a katika elimu ambayo ni muhimu katika kuleta mabadiko ambapo amesema atahamasisha jamii kuhakiisha wasichana waqnapata elimu stahiki.