Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea Kaskazini yaipinga ripoti inayoelezea uvunjifu wa haki za binadamu

Korea Kaskazini yaipinga ripoti inayoelezea uvunjifu wa haki za binadamu

Korea ya Kaskazini imeipinga vikali ripoti iliyotolewa na kamishna huru iliyochunguza juu ya kufanyika kwa vitendo vya uvunjifu wa haki za binadmau na kueleza kwamba ripoti hiyo imejaaa vitu vya kutunga.

Mwanadiplomasia wake mjini Geneva So Se Pyong amesema kuwa wale waliotoa ushahidi mbele ya tume hiyo walikuwa ni wasaliti na ambao walikimbia nchi kutokana na kuhusika katika vitendo vya kihalifu.

Aliishutuma Marekani na mataifa mengine kwa kujaribu kutumia ripoti ya tume hiyo kutaka kuuondosha madarakani utawala halali.

Ripoti hiyo iliyojadiliwa kwenye baraza la haki za binadamu, imesema kulikuwa na matukio ya uvunjifu wa haki za binadamu ambayo mengine yalifanywa kwa mpangilio maalumu