Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haikupunguzii chochote kumpa mwanamke nafasi: Mwanamitindo Flaviana Matata

Haikupunguzii chochote kumpa mwanamke nafasi: Mwanamitindo Flaviana Matata

Wakati mikutano mbalimbali kuhusu hali ya ya wanwake ikiendelea mjini New York Marekani, mwanamitindo nguli wa kimataifa kutoka Tanzania Flaviana Matata ambaye pia anamiliki taasisi iitwayo Flaviana Matata inayotoa misaada ya kielimu, amesema ikiwa wanawake watainuana na kupeana nafasi watapiga hatua kwani kufanya hivyo kunatoa fursa zaidi kwa kundihilo.

Katika mahiojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhudhuria kikao kilichoangazia ushiriki wa wasichana katika masomo ya sayansi, amesema inahuzunisha kuona wanawake wakiwekeana fitina katika kusonga mbele. Hapa anaanza kwa kueleza nafasi ya wanawake katika sayansi.

(SAUTI MAHOJIANO)