Suala la Hakiza Binadamu katika DPRK lizingatiwe haraka: UM

14 Machi 2014

Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu wajibu wa kulinda, Jennifer Welsh, ameelezea kusikitishwa na matokeo ya uchunguzi kuhusu haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, ambayo yaliwekwa bayana mnamo Februari 17, 2014, na ambayo yatawasilishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu.

Kutokana na ushahidi uliokusanywa kutoka kwa wataalam, na waathiriwa na jamaa zao, tume ya uchunguzi ilibaini kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, ukiwemo uangamizaji wa watu, utumwa, utesaji, utoaji mimba wa kulazimishwa, ukatili wa kingono na utapia mlo wa kushurutishwa, umetendeka katika DPRK, chini ya sera zilizowekwa na uongozi wa ngazi ya juu zaidi.

Bi Welsh amesema kuwa uhalifu huo ambao bado unaendelea kwa mujibu wa tume hiyo, unatishia ubinadamu na hivyo unatakiwa kuzingatiwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na wadau wengine. Amesema wakati ulimwengu umeangazia mizozo ya Syria na Jamhuri ya Afrika ya Kati, ushahidi uliotolewa na waathirika wa ukiukwaji wa DPRK unadhihirisha kuwa watu wa DPRK nao wanahitaji hatua za dharura na mathubuti.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter