Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR inakabiliana na hali ya kiafya ya wakimbizi walioko Cameroon

UNHCR inakabiliana na hali ya kiafya ya wakimbizi walioko Cameroon

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR imesema wakimbizi wengi wanaokimbia mapigano huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wanawasili Mashariki mwa Cameroon wakiwa na njaa na hata magonjwakamavile Malaria na utapiamlo.

(Fatoumata Lejeune-Kaba ni kutoka UNHCR)

 “Asilimia 80 ya wanaowasili wana magonjwa kama Malaria, zaidi ya asilimia 20 ya watoto wanaugua utapiamlo tangu wakiwa CAR  wengi wao walilazimika kutemebea kwa miguu kwa miezi na kujificha vichakani bila chakula au majisafi. wengi wamewapoteza jamaa zao kwa njaa njiani au muda mfupi baada ya kuwasiliCameroon. Pia wameathiriwa na yale walioyoyashuhudia  kaskazini magahribi mwa CAR.”