Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Teknolojia kutumika kutokomeza usafirishaji binadamu

Teknolojia kutumika kutokomeza usafirishaji binadamu

Matumizi ya teknolojia mathalnai simu za mikononi ni miongoni mwa m,binu stahiki za kufikisha elimu juu ya ukomeshaji wa biashara haramu ya usafirishaji wa bindamu inayoathiri zaidi wanawake na wasichana.

 Akizungumza na idhaa hii kandoni mwa mkutano wa hali ya wanawake duniani unaondelea mjini New York, Marekani, ulioangazia ukubwa wa biashara hiyo barani Afrika na namna ya kuitokomeza, mkurugenzi mtendaji wa tasisi ya mapambano dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu iitwayo 'The connected hearts" , Nelly Niyonzima amesema  kwa kuwa teknolojia imekuwa barani Afrika ni muhimu ikatumika kufikisha elimu

 (SAUTI NIYONZIMA)

Amesema kwa kushirikiana na mashirika mabliambali yenye uwakilishi katika mikutano inayoendelea hapa mjiniNew Yorkwatahakikisha wanasaidia kuwakomboa wasichana na wanawake ambao wameshasafirishwa na wanahitaji ukombozi

(SAUTI NIYONZIMA)