Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wito watolewa kukabili uhalifu wa kuwanyanyasa watoto kingono

Wito watolewa kukabili uhalifu wa kuwanyanyasa watoto kingono

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uuzaji wa watoto, biashara ya ngono inayowahusisha watoto na watoto kutumiwa katika picha za ngono, Najat Maalla M’jid, ametoa wito ulimwengu ukabiliane na tatizo linaloongezeka la uhalifu wa kuwanyanyasasa watoto kingono.

Mtaalam huyo wa Umoja wa Mataifa amesema watoto wamo hatarini zaidi kunyanyaswa kimapenzi au kuuzwa nyakati za sasa kuliko ilivyokuwa zamani, kwa sababu dunia ya sasa ni ya utandawazi.

Akiiwasilisha ripoti yake ya mwisho kwa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Bi Maalla M’jid ameongeza kuwa mamilioni ya watoto wa kike na wavulana kote duniani ni waathirika wa unyanyasaji wa kingono, hata ingawa tatizo hilo limedhihirika zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Amesema picha za watoto katika ngono zinaongezeka kwenye mitandao ya intaneti, huku waathiriwa wa unyanyasaji huo wakizidi kuwa wadogo, na picha zikiwa za kutisha zaidi.