Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO na Procter & Gamble wazindua kijitabu cha kusaidia vijana barubaru

UNESCO na Procter & Gamble wazindua kijitabu cha kusaidia vijana barubaru

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na kampuni ya Proctar and Gamble wamezindua kijitabu cha kusaidia vijana hao hususan wasichana kukabiliana na kubalehe kwani wamesema kila mwaka wasichana Milioni 50 duniani kote hubalehe lakini kipindi hicho kina mapito makubwa kwani wasichana hukosa mwongozo wa kuwawezesha kuwa imara. Edgar Sandoval ni Makamu Rais wa P&G kuhusu afya kwa wanawake.

(Sauti ya Edgar)

“Na tunajua kubalehe ni hatua ya maisha, ndio, inaleta hamasa! Lakini pia inatisha! Ni wakati ambapo kujitambua na kujiamua kunaweza kuporomoka! Na takwimu zinaonyesha kuwa kujitambua kwa wasichana huporomoka maradufu zaidi kwa wasichana kuliko kwa wavulana.”

Uzinduzi huo ulishuhudia filamu fupi ya shuhuda za wasichana walioanza hedhi baada ya kubalehe wakisema wengine walitengwa kwa fikra potofu kuwa hedhi ya kwanza ni dalili ya kufanya ngono nje ya ndoa, ilihali wengine waliambiwa hedhi siyo kitu cha kumweleza mtu yeyote.