Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madawa ya kulevya yahatarisha afya na maendeleo :UNODC

Madawa ya kulevya yahatarisha afya na maendeleo :UNODC

Utengenezaji pamoja na usafirishaji wa madawa ya kulevya unaendelea kusababisha hatari kubwa kwa afya za watu kila mahali ukiathiri maendeleo endelevu ya nchi na kanda mbalimbali amesema mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na madawa ya kulevya UNODC Yury Fedotov. Taarifa zaidi na Joseph Msami

(TAARIFA YA MSAMI)

Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya madawa ya kulevya ulioanza leo mjini Vienna Austria Bwana Fedotov amewaaambia wshiriki wa mkutano huo kuwa licha ya juhudi nyingi za kupambana na madawa hayo bado kuna megi ya kufanya

Akizungumza katika mkutano huo kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema madawa ya kulevya yanazorotesha nguvu za uchumi na mifumo ya sheria na kutaka nchi kushirikiana katika mapambano hayo.

(SAUTI JAN)

 Mkutano huo ambao pia utaangazia madhara ya afya, juhudi za kikanda za kupunguza usambazaji wa madawa ya kulevya pamoja na utekelezaji wa mikataba ya kuzuia madawa hayo haramu utamalizika tarehe 21 March.