Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wa habari Iraq

UNESCO yalaani mauaji ya waandishi wa habari Iraq

Mkurugenzi Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya wapigaji picha waIraqi wawili.

Wanahabari hao waliokuwa wanafanya kazi katika kituo cha televisheni cha Al-Iraqia waliuwawa wiki iliyopita baada ya shambulizi la mauaji ya kujitoa katika kituo kimoja mjini Hilla.

Bokova alielezea hofu yake huhusu usalama wa wanahabari nchini Iraq na kutolea wito mamlaka kuhakikisha waliotekeleza mauaji hayo wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria.

Kufikia sasa idadi ya wanahabari ambao wameuwa nchini Iraq imefikia 18 tangu kuanza kwa mwaka 2013.