Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi kukutana kujadili tatizo la madawa ya kulevya

Viongozi kukutana kujadili tatizo la madawa ya kulevya

Vingozi mbalimbali duniani wanakutana mjini Vienna Austria kwa ajili ya mkutano wa mjadala kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la mapamabnao dhidi ya dawa za kulevya UNODC, mkutano huo unaoanza hapo kesho March 13 utahusisha watu mashuhuri akiwamo Malkia Silvia wa Sweden pamoja na naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson.

Mkurugenzi Mkuu wa NODC Yury Fedotov amesema ana matumaini mkutano huo utazaa matunda katika kushughulikia tataizo la madawa ya kulevya akisema sio tu kuwa utapitia utekelezaji wa tamko la kisiasa na mpango mkakati lakini pia kusaidia UNODC katika kupaambana na harakati zake siku za usoni.