Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria ya ndoa kikwazo cha maendeleo kwa wanawake

Sheria ya ndoa kikwazo cha maendeleo kwa wanawake

Sheria ya ndoa inayoruhusu wasichana kuolewa katika umri mdogo ni moja ya vikwazo katika utekelazaji wa malengo ya milenia hususani  lengo la tatu la kukuza usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake.

Katika mahojiano maalum na idhaa hii kandoni mwa kikao cha 58 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani mjini New York, Marekani ambapo utekelezaji wa malengo hayo unaangaziwa, waziri wa jinsia wa Malawi  Mary Makungwa amesema nchi hiyo imeanza mchakato wa kubadilisha sheria hiyo.

(SAUTI MAKUNGWA)

"Katika kikao cha bunge kijacho tunaamini kwamba bunge litabadilisha  sheria ya umri wa ndoa kwa kuwa hili limekuwa kikwazo kwa maendeleo ya wanawakwe, tumeakubaliana kupitia viongozi wa dini, makabila kwamba kuwe na nyongeza ya umri wa wasichana kuolewa."

Hata hivyo Bi Makungwa amesema hatua kadhaa zimepigwa nchini Malawi katika  utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia unaofikia ukomo mwak 2015.

(SAUTI MAKUNGWA)

Katika wizara ya jinsia tumejikita katika suala la kubadilisha jamii ambapo tunajaribu kuimarisha maisha ya maskini hususani vijijini katika wilaya tuna hizi progamu na zinaleta mabadiliko. Katika sekta ya kilimo pia tunahakiisha wanawake wanashiriki na hili limeonekana kuwa la manufaa..”