Wanaharakati Uganda wasaka haki mahakama kupinga sheria ya mapenzi ya jinisia moja

Wanaharakati Uganda wasaka haki mahakama kupinga sheria ya mapenzi ya jinisia moja

Takribani wiki tatu baada ya sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja kupitishwa rasmi nchiniUganda, wanaharakati wa haki za binadamu wamekimbilia mahakama ya kikatiba kupinga sheria hiyo. John Kibego wa  Radio washirika ya Spice FM, nchiniUgandana taarifa kamili.

(TARIFA YA JOHN KIBEGO)

Wanaopinga sheria hiyo ni wanaharakati wa haki za binadamu na wasomi wanaojumuisha Prof. Oloka Onyango wa Chuo Kikuu cha Makerere, aliyekuwa kiongozi wa upinzani Prof. Ogenga Latigo na and Andrew Mwenda ambaye ni mwandishi wa habari mkongwe wa zamani.

Wanasema kwamba adhabu kali kama ilivyotolewa katika sheria hiyo ya kupinga mapenzi jinsia moja haiko wazi katika katiba ya jamhuri ya Uganda.

Pia wanataka mahakama ya juu kubana kuchapisha ama kutangaza majina ya watu wanaoshukiwa kuwa ni wapenzi wa jinsia moja.

Kwa mujibu wao, sheria hiyo inakinakandamiza haki ya watu ya faragha, kujieleza, kujumuika na hatimaye kukusanyika.

Sheria ya kupinga mapenzi hayo iliotiwa saini na rais Museveni mwezi uliopita inatoa kifungo cha maisha jela kwa mtu aliyehusika na mapenzi hayo kwa mara zaidi ya moja, na miaka 14 kwa aliyehusika kwa mara ya kwanza.