Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya wanawake ni ya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa:IPU

Idadi ya wanawake ni ya juu zaidi kuwahi kushuhudiwa:IPU

Idadi ya wanawake bungeni kote duniani imeimarika ikifika rekodi mpya ya asilimia 22. Muungano wa wabunge duniani IPU unasema kwamba ongezeko hilo limetokana na uwajibikaji wa kisiasa na nchi binafsi kuhakikisha wanawake zaidi wanateuliwa.

IPU inasema kwamba idadi ya wanawake hususan katika nchi za Marekani na baadhi ya nchi barani Ulaya na Afrika ni ya kutia matumaini. Katika mahojiano maalum na Patrick Maigua wa radio ya Umoja wa Mataifa Jemini Pandya anaelezea hali ilivyo.

(Sauti ya Pandya)

Tumeona ongezeko la alama 1.5  ambayo ni mafanikio kwa wanawake kwa uwakilishi wa wanawake bungeni. Hatujaona ongezeko hilo katika serikali kuu, Marekani ni kinara katika asilimia ya wanawake katika serikali kuu, mawaziri na wabunge. Afrika pia imefanya vyema sana- katika mwaka 2005 bara hilo lilikuwa na chini ya asilimia 10 ya wanawake wabunge sasa wana asilimia 22.5, nchi za  Kaskazini mwa dunia zina mawaziri wanawake sawa na wanaume na wabunge wanawake sawa na  wanaume

Ripoti ya "Wanawake katika ramana ya siasa ya 2014" imezinduliwa Jumanne ya leo hapa  makao makuu ya Umoja wa Matiafa.