Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya kuanza kutambuliwa na kutetewa safari ya albino kujikomboa bado ni ndefu: Mwanaharakati

Licha ya kuanza kutambuliwa na kutetewa safari ya albino kujikomboa bado ni ndefu: Mwanaharakati

Mwanaharakati wa ulemavu wa ngozi, albino ambaye ni afisa katika taasisi ya utetezi wa kundi hilo iitwayo Under the same sun, Ikponwosa Ero amesema licha ya kwamba serikali nyingi duniani hivi sasa zinatambua na kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, bado safari ya ukombozi wa kundi hilo ni ndefu.

Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswizi Bi Ero ambaye ni mlemavu wa ngozi amesema watu wenye uklemavu huo wanaunga mkono pendekezo la baraza la haki za binadamu la kuanzisha chombo cha kutetea haki za kundi hilo.

(SAUTI ERO)