Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CSW58 iangazie madhila yanayokumba wanawake wakiwemo wale wa jamii za kiasili.

CSW58 iangazie madhila yanayokumba wanawake wakiwemo wale wa jamii za kiasili.

Mwaka umeanza na mkutano mwingine wa kutathmini hali ya wanawake duniani umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Ukijulikana kama CSW58, yaani Kamisheni ya hali ya wanawake , mkutano huu hukutanisha viongozi wa serikali na makundi ya kiraia ili kuangalia mustakhbali wa wanawake, na mwaka huu mkutano huu ni adhimu zaidi kwani malengo ya maendeleo ya milenia yanafikia ukomo mwakani! Je nini matarajio? Basi ungana na Assumpta Massoi wa Idhaa katika mahojiano na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.