Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yaliyotokea Maldives yamsikitisha Katibu Mkuu wa UM

Yaliyotokea Maldives yamsikitisha Katibu Mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameeleza masikitiko yake na kitendo cha uamuzi wa mahakama ya juu kabisa nchini Maldives kuwaondoa madarakani mwenyekiti na makamu wa Tume ya uchaguzi nchini humo.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema uamuzi huo wa tarehe Tisa Machi ulioenda sanjari na kumhukumu Mwenyekiti huyo kwa kosa la kudharau mahakama ni jambo la kusitikisha.

Bwana Ban amerejelea umuhimu wa kuheshimu misingi ya mgawanyo wa madaraka, utawala wa kisheria na uhuru wa kikatiba ulioanzisha vyombo husika.

Amewaka viongozi wa kisiasa nchini humo kuheshimu mchakato wa kisiasa na kuruhusu uchaguzi wa bunge kufanyika kidemokrasia na kwa uwazi kwa mujibu wa katiba. Juu ya yote, Bwana Ban amesema ni vyema kabisa utashi wa wananchi wa Maldives ukaheshimiwa wakati wote wa mchakato huo.