Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Šimonović ziarani Ukraine, katika kusaidia kupunguza mvutano

Šimonović ziarani Ukraine, katika kusaidia kupunguza mvutano

Katika kuimarisha hali ya haki za binadamu na kupunguza mvutano unaondelea nchini Ukarine msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Ivan Šimonovićyuko ziarani nchiniUkrainemjini Kharkiv. Joseph Msami na taarifa zaidi

(TAARIFA YA MSAMI)

Katika ziara hiyo Bwana Šimonović anakutana na mamalaka nchini humo kwa lengo kujadili hatua za kuchukua zinazohusiana na haki za binadamu ili kupunguza mvutano nchini humo.

Kadhalika Bwana Šimonović atatumia ziara yake kutathimini hali ya haki za binadmu katika ukanda akitaka kuheshimiwa kwa haki hizo pamoja na kujadili namna Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa inavyoweza kusaidia kuimarisha uwezo pale inapohitajika.

Akizungumzia hatua hiyo msemaji wa ofisi ya haki za binadmau ya Umoja wa Mataifa Ravina Shamdasani anasema

(SAUTI RAVINA)

Kiongozi huyo anatarajia kusafiri hadi jimboni Crimea siku ya jumatano na Liviv siku ya alahamisi na siku ya ijumaa anatarajia kukutana na waandishi wa habari mjini Kiev.