Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu maalum akaribisha hatua ya Mauritania kupinga utumwa

Mratibu maalum akaribisha hatua ya Mauritania kupinga utumwa

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya maswala ya utumwa Bi Gulnara Shahinian amekaribisha hatua ya Mauritania kupitisha pendekezo la Ofisi ya Kamishna ya haki za binadamu kama hatua muhimu katika vita dhidi ya utumwa.

Bi Shahinian, amesema kwamba hatua hiyo iliyochukuliwa na Mauritania Machi 6 2014 ya kupitisha mapendekezo ya 2010 sio tu ishara bali pia inafungua njia mpya katika kumaliza utumwa kabisa.

Ameongeza kuwa anaamini kwamba serikali itatekeleza kikamilifu mapendekezo kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii ili kuhakikisha kwamba kunapatikana mabadiliko ya kudumu. Tamko hili limekuja baada ya wiki moja tangu ziara ya mratibu maalum huyo nchini humo ya kuzungumizia maendeleo yaliofikiwa tangu kupitishwa kwa mapendekezo ya awali ambayo ni pamoja na kurekebisha sheria ya 2007 kuhusu maelezo ya utumwa ili kuhakikisha utekelezajj na kutoa msaada wa kijamii na kiuchumi kwa waathirika ili kuwawezesha kutengamana na jamii.

 Bi Shahinian atawasilisha ripoti kwa Kamisna ya haki za binadamu mwezi Septemba mwaka huu.