Mtaalam wa Umoja wa Mataifa ataka watetezi wa haki za binadamu walindwe

Mtaalam wa Umoja wa Mataifa ataka watetezi wa haki za binadamu walindwe

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu Margeret Sekaggya, amesema kuwa anaingiwa na hali ya wasiwasi mkubwa kutokana na watetezi hao wa haki wanavyopata shida. Taarifa zaidi na alice Kariuki

(Taarifa ya Alice)

 Akiwasilisha ripoti yake ya kila mwaka kuhusiana na nchi alizotembelea mwaka uliopita, mtaalam huyo amesema kuwa watu waliojitoa mstari wa mbele kutete haki za binamau wanakabiliwa na vitisho juu ya usalama wa maisha yao.

Alisema kuwa vitisho hivyo vinakwenda mbali zaidi kwani hata familia zao zimetumbukizwa kwenye hali hiyo.

Kaika kipindi cha mwaka uliopita, mtaalamu huyo alizitembelea nchi za Korea na Togo kwa ajili ya kutathmini hali ya haki za binadamu.

Akielezea zaidi kuhusiana na ziara yake nchini Korea mtaalamu huyo alisema kuwa watetezi wengi wa haki za binadamu nchini humo wanakabiliwa na hali ngumu kutokana na mazingira wanayofanyia kazi kuwa siyo rafiki.

Kuhusu Togo alisema kuwa changamoto kubwa iliyoko nchini humo ni kukosekana kwa mihimili ya kisheria.

(Sauti ya Margaret)