Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya wanawake duniani yamulikwa Maziwa Makuu Afrika

Siku ya wanawake duniani yamulikwa Maziwa Makuu Afrika

Tarehe Nane Machi kila mwaka ni siku ya wanawake duniani! Ujumbe wa mwaka huu ni Usawa kwa wanawake Maendeleo kwa Wote! Ujumbe huo umepigiwa chepuo kila kona ya dunia kwa kutambua kuwa iwapo wanawake watapatiwa fursa zaidi iwe katika sekta  za kijamii, kiuchumi au kisiasa, manufaa yanayopatikana ni kwa jamii nzima. Hii ni kwa kuzingatia nafasi adhimu kwenye kaya zao na jamii kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anasema mwaka huu wanaangazia usawa kwa wanawake na watoto wa kike, siyo eti kwa sababu ni kwa minajili ya usawa na haki ya msingi ya kibinadamu, bali ni kwa kuwa maendeleo kwenye maeneo mengi yanategemea suala hilo. Je fursa zikoje? Usawa upo na zipi ni changamoto? Katika makala hii basi tunajikita Maziwa Makuu ya Afrika.