Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mama yangu hakuwa amesoma lakini alihakikisha naingia sekondari: Hajjat Amina Mrisho Saidi

Mama yangu hakuwa amesoma lakini alihakikisha naingia sekondari: Hajjat Amina Mrisho Saidi

Kuwapatia wanawake fursa katika nyanja zote ni muhimu kwa maendeleo ya kaya zao na hata taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imejidhihirisha kwa Hajjat Amina Mrisho Saidi, Kamishna wa Sensa Tanzania mwaka 2012 ambaye baada ya kumaliza elimu ya msingi alijikita katika kuchunga mbuzi huko kwao mkoani Arusha akidhani ndoto ya elimu ya sekondari imetwama! Hata hivyo jitihada za mama yake mzazi na zake yeye binafsi pamoja na serikali zilimwezesha kufika alipo sasa. Hajjat Amina alifunguka bayana katika mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu siku ya wanawake duniani ambapo anaanza kwa kuelezea familia yao..