Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

New York katika pilka pilka za kuadhimisha Siku ya Wanawake

New York katika pilka pilka za kuadhimisha Siku ya Wanawake

Wakati huo huo, shughuli nyingine zimepangwa kufanyika hapa mjini New York kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.

Shughuli hizo ni pamoja na maandamano ya wanawake mashuhuri, wakiwemo mkewe Katibu Mkuu Bi Ban Soon-taek, nyota nyota wa mitindo, Naomi Campbell na mwanamuziki na mwigizaji Monique Coleman, ambayo yatalenga kuchagiza uelewa kuhusu haja ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake.

Hapo kesho, picha na maandishi yenye ujumbe wa usawa na maendeleo vitaonyeshwa kwa siku nzima kupitia runinga ya Nasdaq, kwenye eneo maarufu la Time Square.