Wanawake, vijana na mashirika ya kiraia yapatiwe fursa zaidi ajenda ya baada ya 2015

7 Machi 2014

Ratiba ya shughuli za Umoja wa Mataifa imesheheni ajenda kuhusu wanawake kuelekea kilele cha siku hiyo duniani kesho Machi Nane. Mathalani asubuhi kumefanyika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu mchango wa wanawake, vijana na mashirika ya kiraia kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015. Taarifa kamili ya Grace Kaneiya:

(Taarifa ya Grace)

Tarja Halolen, Rais wa kwanza mwanamke waFinlandaliongoza kikao hicho kilichotaka mchango wa makundi hayo utumike vyema kwenye maandalizi  ya ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 akisema kuwa iwapo yataenguliwa basi hakuna kinachoweza kufanikiwa.

Amesema uzoefu umeonyesha uwekezaji kwa vijana na usawa kwa kijinsia umepunguza umaskini, vifo vya watoto na kuchochea maendeleo na kwamba wanawake wakienguliwa nusu ya watu duniani wameenguliwa..

 (Sauti ya Tarja)

“Kwa jamii kufanikiwa, tunahitaji uwezeshaji wa  wanawake, usawa wa kijinsia na ulinzi wa haki za kijinsia na uzazi. Kwa kufanya hivyo tunaweza  kuimarisha maendeleo endelevu.”