Vijana wanajua wanachotaka: Ashe

6 Machi 2014

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa John Ashe amezungumza katika mkutano uliojadili mchango wa wanawake, vijana na asasi za kiraia kuelekea ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015 na kusema vijana kote duniani wanajua wanacghotaka na kuhitaji.

Bwana Ashe amesema wakati malengo ya maendeleo ya milenia yakiwa yanaelekea ukomo wake mwak 2015 ikumbukwe kuwa zaidi ya watu bilioni moja duniani ni vijana ambapo miongni mwao ni barubaru na hivyo na ni mtaji mkubwa kwa dunia.

(SAUTI ASHE)

Wakati mara nyingi hukataliwa uwekezaji na fursa za kutumiwa kwa uwezo wao kamili , ikiwa ni kwasababu ya ukosefu wa ajira na fursa za elimu, mzigo wa magonjwa au ndoa za utotoni, wanajua wanachotaka na kuhitaji . Elimu bora na huduma za afya, fursa za ajira, kulindwa dhidi ya unyanyasaji , undolewaji wa vikwazo vinavyozuia ujumuishwaji na ushirikishwaji na serikali ya uwazi na ukweli

Balozi Ashe amesema kote duniani vijana wameonyesha kuchochea mabadiliko katika vuguvugu la kijamii na kisiasa kuanzia Mashariki ya mbali, Ulaya mashariki, Amerika ya Kusini na Afrika.