Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake kujumuishwa katika malengo endelevu ya milenia baada ya 2015

Ukatili dhidi ya wanawake kujumuishwa katika malengo endelevu ya milenia baada ya 2015

Vita dhidi ya ukatili kwa wanawake utakuwa ni sehemu ya malengo yanayopwa kipaumbele kuelekea malengo ya maendeleo ya milenia baada ya mwaka 2015 amesema mkrugenzi mkuu wa kitengo cha masuakla ya wanawake katika Umoja wa Mataifa Phumzile Mlambo-Ngcuka

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Bi Ngcuka amesema suala hili ni mtambuka akitolea mfano namna linavyoingiliana na sekta za elimu na afya.

(SAUTI NGCUKA)

"Pia tunaona kuwa hii ni moja ya changamoto amabayo haiytakuw jukumu la wanwake pekee bali mtambuka ikiwa unahusika na elimu, kwa kuwa sehemu ya ukatili ni kuwatoa shuleni wasichana kutokana na mimba za mapema. Katika afya kuna mambo magumu ambapo wataalamu wa sekta hii wanakutana nayo yanayohusika na ukatili dhidi ya wanawake."

Kadhalika mkuu huyo wa kitengo cha wanawake katika Umoja wa Mataifa amesema kinacchomfariji ni takwimu zinazoonyesha kuwa kuwa ikiwa wanawake watajumuishwa katika nguvu kazi ukujai wa uchumi utaongezeka

(SAUTI NGCUKA)

"Kinachofurahisha katika karne tatu zilizopita ni muendelezo wa takwimu unaotoa uthibitisho kuwa usawa kwa wanawake ni maendeleo kwa wote, mfano takwimu zinazosema kuwa ikiwa wanawake watapewa pembejeo sawa za kilimo, zaidi ya watu milioni 150 watakuwa na uhakika wa chakula au ukweli kwamba kamouni ambazio zimejumuisha jinsia zote zimefanya vizuri zaidi na kuongeza faida kwa asilimia 34. Pia ikiwa wanawake wote watahusishwa katika nguvu kazi uchumi ungekuwa kwa asilimia 12."