Gharama zisiwe kikwazo kuboresha mfumo wa kukusanya takwimu:

6 Machi 2014

Mkutano wa 45 wa Umoja wa Mataifa kuhusu takwimu unaendelea mjini New York, Marekani ambapo wataalamu wa takwimu kutoka nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea wanajadili mustkhbali wa jukumu la takwimu katika ajenda ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 malengo ya maendeleo ya milenia yanapofikia ukomo.

Miongoni mwa washiriki ni Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dokta Albina Chuwa na Kamishna wa sense nchini humo mwaka 2012 Hajjat Amina Mrisho Saidi ambao katika mahojiano na Assumpta Massoi wa idhaa hii wameeleza fursa zinazopaswa kutumia kuboresha ukusanyaji wa takwimu na halikadhalika kurahisisha matumizi yake kwa mwananchi wa kawaida. Hapa Dokta Chuwa anaanza kwa kuzungumzia lengo la mkutano huo.