Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Cambodia yapongezwa kwa kufanyia marekebisho ya mfumo wa uchaguzi

Cambodia yapongezwa kwa kufanyia marekebisho ya mfumo wa uchaguzi

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Cambodia, Surya P. Subedi, amelipongeza taifa hilo kwa makubaliano ya vipengee vitano kuhusu marekebisho ya mfumo wa uchaguzi, ambayo yalifikiwa na vyama viwili vikubwa vya kisiasa bungeni.

Amekaribisha pia hatua ya kuondoa marufuku ilowekwa mnamo tarehe 5 Januari 2014 dhidi ya kufanya maandamano, akisema hatua ya kupiga marufuku maandamano ilienda kinyume na wajibu wa Cambodia wa kulinda haki za binadamu chini ya Mkataba wa Kimataifa na Katiba yake yenyewe.

Hata hivyo, mtaalam huyo wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa serikali ya Cambodia kuheshimu haki ya kujieleza na uhuru wa watu kufanya mikutano.