Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikwazo vya silaha Somalia

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikwazo vya silaha Somalia

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limepitisha azimio la kuongeza muda wa vikwazo vya silaha nchini Somalia, lakini likaruhusu serikali ya Somalia kununua silaha kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taifa hilo, hadi tarehe 25 Oktoba mwaka huu wa 2014.

Azimio hilo limetokana na kufanyiwa marekebisho azimio namba 2093 la tarehe 6 Machi, 2013, ambalo liliondoa vikwazo vingi ambavyo vilikuwa vimewekewa uagizaji wa silaha ndogondogo za kutumiwa na jeshi la taifa la Somalia.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya UM nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay, anatarajiwa pia kuwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ofisi hiyo.

Mkutano wa leo pia unatarajiwa kuongeza muda wa jopo la wataalam wa kamati ya vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, na kusikia ripoti kuhusu mpango wa kuteketeza silaha za kemikali Syria.