Nchi kusaidiwa kufikia malengo ya uchumi unaojali mazingira

5 Machi 2014

Kumekuwa na mikakati ya kuziwezesha nchi ziweze kufikia shabaha ya kuendesha uchumi unaojali mazingira  ifikapo mwaka 2020.

Mipango hiyo ni pamoja na kuziwezesha nchi kuzingatia sera ambazo zitatilia mkazo utekelezaji wa miradi endelevu. Nchi ambazo zinatazamiwa kupigwa jeki ni pamoja na Burkina Faso, Peru, Mauritius, Mongolia,na Senegal.

Ili kufanikisha mkakati nchi wahisani zimetangaza kutenga kiasi cha dola za Marekani milioni 11 kugharimia miradi ya maendeleo.Baadhi ya nchi zilotoa fedha hizo ni pamoja na Finland.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud