Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya Sudan Kusini yanakwamisha misaada kwa watoto

Mapigano mapya Sudan Kusini yanakwamisha misaada kwa watoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema mapigano mapya huko Sudan Kusini yanakwamisha jitihada zake za kupeleka misaada kwa watoto.

Msemaji wa shirika hilo mjini Geneva, Uswisi, Patrick Mccormick amesema mamia ya maelfu ya wanawake, wanauame na watoto hawawezi kufikiwa ili kupatiwa misaada ya dharura ikiwemo maji safi na salama na huduma za kujisafi.

Amesema jitihada za kufikisha misaada hukumbwa na zahma kila siku. UNICEF inasema zaidi ya Laki tatu na Nusu wako hatarini kukumbwa na magonjwa kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ukosefu wa fedha. Kati ya dola Milioni 75 zilizoomba ni dola Milioni 20 za usaidizi zilizokwishapatikana.